March 19, 2015


Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amesema nafasi kadhaa walizopoteza, zimechangia wao kupoteza mchezo dhidi ya Mgambo.


Simba imekumbana na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Mgambo katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani Tanga, jana.

Kopunovic raia wa Serbia, amesema walipata nafasi nyingi za wazi, lakini hawakuzitumia.

“Angalau tungepata nafasi mbili, ingekuwa lahisi kuuamua mchezo. Hatukufanya hivyo.

“Mgambo si timu nzuri ya kutisha, ila walicheza kwa nguvu kibabe wakitaka kutuvuruga. Mwisho wamefanikiwa, hii imenivuruga sana,” alisema Kopunovic.

Simba ilifungwa bao la pili  kwa penalti baada ya kipa wao Ivo Mapunda kulambwa kadi nyekundu kwa kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Mgambo.]

2 COMMENTS:

  1. Tuache kutafuta visingizio, ndo maana tukienda nje tukishindwa tunasingizia fitina na tukishinda basi tulicheza vizuri na kufuata maelekezo. Mgambo walicheza kibabe, mbona hawakupata kadi nyekundu!? au tuseme refa aliwapendelea!?

    ReplyDelete
  2. HAPO MIE HOI,NA NILIWACHEKAJE SIMBA!
    MECHI NYINGINE MNAAMINI UCHAWI MPAKA MNAKATAA KUINGIA VYUMBANI NA KUVALIA NGUO KWENYE BASI,( KAMA MECHI HII NA MGAMBO) HII YOTE NI KUAMINI UCHAWI MKUBALI, MSIKUBALI.
    MBAYA ZAIDI IVO UKASAHAU NA ILE IMANI YAKO"PROTECT ME JESUS" NAKUAMINI KUROGWA,NAAMINI MUNGU KAKUONYESHA NA UTAJIFUNZA.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic