Bondia Karama Nyilawila ametamba kuwa
mpinzani wake Thomas Mashali amekimbia kwa kuwa alijua atakutana na kifo.
Nyilawila amesema hivyo baada ya Mashali
kutotokea wakati wa kupima uzito kabla ya pambano lao kesho.
“Alijua kifo kinamkuta, alipiga sana kelel.
Sasa yuko wapi,” alitamba Nyilawila.
Taarifa zilieleza Mashali ameshindwa kutokea
kwa kuwa ni majeruhi baada ya kucheza mapambano mawili mfululizo ndani ya mwezi
mmoja.
Wawili hao walitakiwa kupambana kesho katika
pambano la kumaliza ubishi kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar.







0 COMMENTS:
Post a Comment