| MAUGO (KULIA) NA KASEBA WAKATI WAKIPIMA UZITO. |
Bondia mwenye maneno mengi, Mada Maugo amesema kipigo atakachompa Japhet Kaseba katika pambano lao la kesho ni zawadi kwa watu wa eneo la Rorya mkoani Mara.
Kaseba na Maugo wanakutana kesho katika pambano linalosubiriwa kwa hamu na wadau wa ngumi.
Wawili hao watapambana katika pambano la utangulizi kabla ya Mohammed Matumla hajapanda ulingoni kumvaa Mchina.
Kwa upande wake Kaseba, alisema amejiandaa vilivyo, hivyo hana hofu hata kidogo na kelele za Maugo ambazo anazifani na zile za chura.







0 COMMENTS:
Post a Comment