March 6, 2015

MARA KADHAA, MANJI HUZUNGUMZA NA WACHEZAJI WAKE. HII ILIKUWA MIAKA MINNE ILIYOPITA.
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji anatarajia kuungana na wachezaji wake walioko kambini mjini Bagamoyo, leo.


Yanga ipo kambini katika hoteli ya Kiromo kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wake wa jadi Simba itayopigwa Jumapili.

Manji atatua kambini leo Ijumaa na iwapo atabanwa na kazi basi piga ua lazima kesho Jumamosi atimize ahadi yake hiyo.

“Pamoja na kikosi kuonekana kuwa kizuri, lakini mwenyekiti ameona kuna umuhimu wa kuzungumza na vijana wake kwa kina zaidi japokuwa haijafahamika atawaahidi nini,” kilisema chanzo.


Msimu uliopita timu hizo zilitoshana nguvu kwa mabao 3-3 mzunguko wa kwanza kabla ya kutoa sare tena ya bao 1-1 kwenye mzunguko wa pili huku msimu huu mzunguko wa kwanza zikitoka suluhu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic