| MSUVA AKIRUKA DARUGA LA HARUNA SHAMTE WA JKT... |
Mshambuliaji kinda wa Yanga, Simon Msuva amefikisha mabao
11 na kumvuka Didier Kavumbagu wa Azam FC.
Msuva amefunga mabao mawili katika mechi ya Yanga dhidi
ya JKT wakati wakishinda kwa mabao 3-1.
Pamoja na mabao hayo, Msuva ameonyesha yuko fiti katika
kiwango ambacho ni bora kabisa.
Fitness si katika kumiliki mpira pekee, lakini hali ya
kujiamini, hamu ya kutaka kufunga na pia msaada kwa timu.
Uchezaji wa Msuva unaonyesha ni mchezaji aliyekamilika na
anayeweza kuwa msaada kwa kikosi chake.







0 COMMENTS:
Post a Comment