March 15, 2015


Simba wametoa pongezi kwa watani wao wa jadi Yanga kutokana na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.


Yanga imeshinda kwa mabao  hayo na kujiweka katika nafasi nzuri katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully amesema kwa niaba ya Rais wa Simba, Evans Aveva wanaipongeza Yanga.

“Yanga ni wawakilishi wa nchi katika michuano ya kimataifa. Hakika wanastahili pongezi kutokana na kufanya vema.

“Inapofikia katika suala la nchi, si vibaya kuwapongeza. Tukirudi kwenye ligi basi upinzani unaendelea.

“Ndiyo maana leo tulikuwa uwanjani kushuhudia Yanga wakipambana na walifanya vema kwa kweli,” alisema Tully.

Yanga imeitandika FC Plutinum kwa mabao hayo matano katika mechi nzuri ya kuvutia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic