March 27, 2015


Suala la mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe kumshika korodani beki wa Simba SC Murshid Juuko limepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu.


Uamuzi wa kulipeleka suala hilo kwenye kamati ya nishamu umefikiwa baada ya Kikao cha Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania  kilichoketi jumanne ya tarehe 24, Machi 2015 jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimepitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa na kutoa adhabu kwa wachezaji na vilabu vya Ligi Kuu ya Bara.

Lakini suala hilo la Tambwe raia wa Burundi kumshika beki huyo wa Simba kutoka Uganda, linakwenda kwenye kamati ya nidhamu.

Tambwe alibambwa 'live' akifanya hivyo kupitia picha iliyopigwa na gazeti namba moja la michezo nchini la Championi.


Picha ya Championi ilichapisha Tambwe akiwa anamvuta korodani beki huyo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic