Straika wa Simba, Ibrahim Ajibu,
anayefanya vizuri kwa sasa, ametangaza dhamira yake ya kutaka kutwaa kiatu cha
ufungaji bora wa ligi msimu huu, hivyo akatoa tahadhari ya ushindani huo kwa
kinara wa mabao mpaka sasa, Mrundi, Didier Kavumbagu anayekipiga Azam FC.
Ajibu alifunga ‘hat-trick’ kwenye
ushindi wa mwisho wa Simba dhidi ya Prisons wa mabao 5-0 kabla ya mchezo wao wa
jana dhidi ya Yanga, akafanikiwa kufikisha idadi ya mabao matano akiwa nyuma kwa
mabao manne kwa Kavumbagu mwenye tisa.
“Ni kazi kubwa kwenye ligi kama hii
kuibuka mfungaji bora lakini kama mtu una nia inabidi kujitahidi zaidi, naamini
nitaweza kuchuana na Kavumbagu na wengine wenye mabao mengi mpaka nitimize nia
yangu ya kutaka kuwa mfungaji bora msimu huu na kuisaidia timu yangu kukaa
kwenye nafasi nzuri,” alisema Ajibu.
Wachezaji wengine waliomzidi idadi ya
mabao Ajibu ni pamoja na Rashid Mandawa (Kagera-8), Simon Msuva (Yanga-7),
Abasirim Chidiebere (Stand-7), wengine ni Samuel Kamuntu (JKT), Ame Ali
(Mtibwa), Kipre Tchetche (Azam), wote wana mabao sita.
0 COMMENTS:
Post a Comment