Straika wa Yanga, raia wa
Burundi, Amissi Tambwe, amedai hivi sasa hajui cha kufanya ili kuhakikisha
anapata haki yake ambayo anaidai Simba baada ya kumvunjia mkataba wake na
kushindwa kumlipa na kuamua kwenda kuomba msaada Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) ambako nako mambo yamezidi kuwa magumu.
Tambwe anaidai Simba zaidi ya dola
6,000 (Sh milioni 11), ambazo klabu hiyo inatakiwa kumlipa baada ya kuvunja
naye mkataba katika kipindi cha usajili cha dirisha dogo kutokana na kile
kilichodaiwa kuwa kiwango chake kimeshuka.
Tambwe amesema kuwa mpaka sasa hajui afanye nini ili aweze kupata haki yake
hiyo ambayo anasatahili kupewa na Simba baada ya kumtimua wakati alikuwa bado
na mkataba.
“Baada ya Simba kunizungusha huku na
kule bila ya kunilipa haki yangu, niliamua kwenda TFF ambako nilipeleka nyaraka
zote kuhusiana na hilo lakini nako naona kama hakuna msaada.
“Hakika nachanganyikiwa kwani haki
yangu inaweza kupotea hivihivi,” alisema Tambwe.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa TFF, Selestine
Mwesigwa, ameliambia Championi Jumatatu kuwa, suala hilo lipo mikononi mwao na
watalifanyia kazi, hivyo Tambwe anatakiwa kuwa mtulivu.
“Tambwe awe mtulivu tu kwani suala
lake hilo hivi sasa lipo mikononi mwetu na muda ukifika litafanyiwa kazi,”
alisema Mwesigwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment