Na Saleh Ally
MECHI ya watani wa jadi,
Yanga dhidi ya Simba ambao ni ‘dugu’ moja, kila inapopigwa inakuwa na jambo
lake ambalo linabaki kuwa gumzo miaka nenda rudi.
Kwa kifupi, wanapokutana
watani Simba na Yanga, basi lazima kuwe na ‘surprise’ ya siku kwa aina yoyote
ile.
Mechi ya kesho Jumapili
inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka huku kukiwa na rekodi kibao
nyuma kabla ya watani hao kukutana leo.
Tuanzie msimu wa wa 2011/12
hadi mechi hiyo ya kesho inakuwa ni mechi ya nane kwa kuwa Yanga na Simba
zimeshakutana mara saba katika Ligi Kuu Bara.
Kila msimu, Yanga na Simba
zinakutana mara mbili katika mechi za Ligi Kuu Bara. Misimu mitatu maana yake
mechi sita na msimu huu zimekutana mara moja na kutoka sare ya bila kufungana.
Katika mechi saba ambazo
zimecheza katika misimu minne, inaonekana wachezaji wa kigeni ndiyo wenye
bahati zaidi ya kutikisa nyavu katika mechi za watani wa jadi hata kuliko
wenyeji.
Katika mechi hizo saba,
wageni ndiyo wenye mabao mengi zaidi kuliko wenyeji na waliotikisa nyavu hizo
wanatokea katika nchi za Zambia, Uganda, Burundi na DR Congo.
Ukianzia msimu wa 2011-12,
jumla ya mabao 18 yamefungwa na wageni wamefunga 11 huku wenyeji au wazawa
wakiwa na 6, hii ni sehemu ya kuonyesha kweli wana bahati zaidi na mechi ya
watani.
Msimu wa 2011-12, mechi
mbili zilikuwa hivi. Ile ya kwanza Yanga ilishinda bao 1-0, mfungaji akiwa
Davies Mwape, raia wa Zambia. Mechi ya pili, Yanga ikakutana na kipigo cha
kihistoria cha mabao 5-0.
Mabao matano ya Simba siku
hiyo, manne yalifungwa na wageni ambao ni Emmanuel Okwi (mawili), Patrick
Mafisango (DR Congo, lakini alichukua uraia wa Rwanda), Felix Sunzu (Zambia) na
mwenyeji pekee aliyefunga siku hiyo ni kipa Juma Kaseja.
Msimu wa 2012-13, mechi ya
kwanza ilikuwa sare ya bao 1-1, wenyeji wakitamba kwa Amri Kiemba kuanza
kuifungia Simba na Simon Msuva akasawazisha. Mechi ya pili, Simba ikalala 2-0,
Mrundi Didier Kavumbagu na Mganda Hamisi Kiiza wakifanya yao.
Ukafuatia msimu wa 2013-14,
mechi ya kwanza, Yanga ikatangulia hadi mapumziko ikiwa na mabao matatu ya
Kiiza (mawili) na Mrisho Ngassa. Simba ikasawazisha yote kupitia Gilbert Kaze
(Burundi), Joseph Owino (Uganda) na Mtanzania Betram Mwombeki.
Ziliporudiana
sare nyingine, safari hii ikiwa ni bao 1-1 akianza kufunga Haruna Chanongo na
Simon Msuva akasawazisha ‘jioni’.
Kwa misimu hiyo mitatu,
zikawa zimekamilika mechi sita na msimu wa nne ni huu wa 2014-15 na mechi ya
kwanza haikuwa na mabao yaani sare ya 0-0.
Mechi ya pili ni ngumu,
kila upande unachoangalia ni kupata pointi tatu. Suala la wageni kufunga au
wenyeji halitiliwi mkazo kwa timu hizo, muhimu ni ushindi.
Lakini halibadilishi kuwa
kweli wageni wana bahati zaidi kwa kuwa katika mechi saba tu wamefunga mabao 11
huku wenyeji wakifunga 7 tu.
Katika mechi hiyo pia sare
zimekuwa nyingi zaidi, kwani katika mara saba walizokutana, Yanga imeshinda
mara mbili, imepoteza moja na sare nne.
Wakati Simba imepoteza mara
mbili, sare nne na imeshinda mara moja, mara ya mwisho kuifunga Yanga katika
Ligi Kuu Bara ikiwa ni ile mechi ya 5-0, mechi ilipopigwa Mei 6, 2012.
Kesho kwa upande wa Simba
wana Waganda tu ambao ni Okwi, Simon na Danny Sserunkuma, Juuko Murshid na
Joseph Owino wakati Yanga wamechanganya uraia wakiwa na Mbuyu Twite na Haruna
Niyonzima (Rwanda), Kpah Sherman (Liberia), Amissi Tambwe (Burundi) wakati
Andrey Coutinho raia wa Brazil atakuwa jukwaani kutokana na majeraha.
Washambuliaji kama Elius
Maguri, Ibrahim Ajib ‘Kadabra’, Ramadhani Singano ‘Messi’ watakuwa na kazi ya
kuonyesha hata wenyeji wanaweza kufunga mabao mengi zaidi.
Kwa upande wa Yanga pia,
Simon Msuva, Mrisho Ngassa, Hussein Javu na wengine, pia wana nafasi hiyo ya
kubadilisha wageni kutawala zaidi.
MECHI:
2011/2012
Oktoba 29, 2011
Yanga 1- 0 Simba
Mwape 72
Mei 6, 2012
Simba 5-0 Yanga
Okwi 1&62,
Sunzu 53,
Kaseja
66
Mafisango 71
2012/13
Oktoba 3, 2012
Yanga 1-1 Simba
Taifa
Bahanuzi 65 Kiemba 4
Mei 18, 2013
Simba 0-2
Yanga
Taifa
Kavumbagu, Kiiza
2013-14
Oktoba 20, 2013
Simba
3-3
Yanga
Taifa
Mwombeki 53 Ngassa
15, Kiiza 35&45
Owino 60, Kaze84
Aprili 19, 2014
Yanga
1-1 Simba
Taifa
Simon Msuva 86 Haruna
Chanongo 75







0 COMMENTS:
Post a Comment