April 24, 2015


Aliyewahi kuwa kocha wa straika wa Simba, Dan Sserunkuma, Mathias Lule amewanyooshea kidole viongozi wa Simba katika kushuka kwa kiwango cha straika huyo na mdogo wake, Simon Sserukuma ambao wameshindwa kuendana na kasi ya Ligi Kuu Bara.


Lule ambaye ni kocha wa Stand United, amesema Simba inahusika kwa asilimia kubwa kwa kudai kuwa wameathirika kisaikolojia kutokana na maneno mabaya yanayosemwa.
 
LULE (KULIA) AKIZUNGUMZA NA KOCHA WA YANGA, HANS VAN DER PLUIJM.
“Hunidanganyi chochote juu ya Dan, nimekuwa naye tangu utotoni, mpaka anakwenda katika akademi huko Sweden. Hakuna fowadi wa kufunga kama yeye, lakini wao ndiyo wamemharibu kisaikolojia kutokana na haya maneno mabaya yanayosemwa juu yake.

“Hata suala la uchawi linachangia. Kwa muda niliokaa Tanzania timu zinawekeza nguvu kwenye uchawi, kitu ambacho ni kipya kwa wachezaji wa Kiganda,” alisema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic