Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu Simba, Mzambia,
Patrick Phiri, ametamka wazi kuwa aliona mapema kuwa kikosi cha Yanga kitaibuka
na ubingwa wa ligi kwa msimu huu kutokana na kasi ambayo walianza nayo tangu
mwanzo wa msimu.
Phiri, mpaka sasa bado hajafanikiwa kupata
timu ya kuifundisha tangu alipotupiwa virago Desemba, mwaka jana ambapo kwa
sasa nafasi yake imechukuliwa na Mserbia, Goran Kopunovic.
Akizungumza kutoka nchini Zambia, Phiri alisema
kuwa aliona tangu awali kuwa kikosi hicho kitatwaa ubingwa kutokana na
maandalizi yake katika michezo yao ambapo walikuwa wanacheza huku wakitafuta
ushindi katika michezo yao.
“Niliona tangu mapema kuwa Yanga wanaweza
kuibuka mabingwa kutokana na kasi waliyoanza nayo mwanzoni tu mwa msimu,
walikuwa moto na walikuwa wanaonyesha kuwa wana uchu wa kutaka kuibuka na
ubingwa.
“Walionekana kuwa bora sana tangu msimu
unaanza na wanastahili hiki ambacho wamekipata, lakini pia wakumbuke kuwa wao
siyo bora zaidi ya Simba kwani wamefanikiwa kuzifunga timu zote kasoro hiyo
pekee,” alisema Phiri ambaye ana rekodi ya kipekee ndani ya kikosi cha Simba
kwa kuifundisha msimu mzima bila kupoteza hata mchezo mmoja.
Kikosi hicho cha Yanga kinachonolewa na
Mholanzi, Hans van Der Pluijm, kilitwaa ubingwa wake wa 25 juzi Jumatatu, baada
ya kuipa kipigo kitakatifu timu ya Polisi Moro cha mabao 4-1 na kufikisha
pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa.
Ndio kusema na yeye sio bora kwa kuwa alifungashiwa virago na Simba?
ReplyDelete