Uongozi wa Yanga FaceBook Family umeonyesha
mfano kwa makundi ya mashabiki baada ya kujitokeza na kuwatuza wachezaji wa
Yanga.
Uongozi wa kundi hilo la mashabiki wa Yanga
ulitoa tuzo kwa wachezaji, makocha na watu wengine wa benchi la ufundi akiwemo
daktari, Juma Sufiani.
Utoaji tuzo hizo ulifanyika jana katika mazoezi
ya Yanga kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
SALEHJEMBE inawapongeza Yanga FaceBook Family
kwa uamuzi wao wa kutambua mchango wa wachezaji wao.
0 COMMENTS:
Post a Comment