Bayern Munich wameng’olewa
kwenye michuano ya Kombe la Ujerumani na wapinzani wao wakubwa Borussia
Dortmund ambao sasa wametinga fainali.
Bayern wameng’olewa kwa
penalti 3-2 huku Xabi Alonso, Phillip Rahm wakikosa baada ya kuteleza. Dortmund walikuwa ugenini jijini Munich.
Halafu kipa nyota, Emmanuel
Neuer ambaye aliokoa penalti moja, naye akakosa na Dortmund ikasonga.
Dakika 90 za mechi hiyo ziliisha kwa sare ya bao 1-1, Dortmund wakisawazisha kupitia Aubameyang baada ya Robert Lewandowski kufunga la kuongoza kwa Bayern.
Sasa Dortmund inasubiri mshindi kati ya Werder Bremen dhidi ya Arminia ambaye atacheza naye fainali.
0 COMMENTS:
Post a Comment