April 29, 2015




Na Saleh Ally
CHELSEA inakutana leo katika mechi ngumu dhidi ya Leicester City katika mchezo muhimu kwa kila timu kwenye Ligi Kuu England ‘Premier’.


Iwapo Chelsea watashinda, basi litakuwa ni pigo muhimu la mwisho kwao katika ligi hiyo na wanaweza kusema wao ni mabingwa kwani wanaweza kutawazwa kutwaa taji kwa kukaa pembeni bila ya kucheza huku wakimuombea njaa ‘adui’ Arsenal.

Chelsea ikishinda mechi ya leo, itafikisha pointi 80, Man City ambao ni mabingwa watetezi watakuwa wamevuliwa rasmi taji. Kwani kwa pointi zao, 67, wakishinda mechi zao nne zilizobaki watakuwa na pointi 79.

Arsenal watabaki pekee kuwa tatizo kwa Chelsea kwa kuwa kwa pointi zao 67, wakishinda mechi zao tano zilizobaki watakuwa na uwezo wa kufikisha pointi 82. Kama kweli Chelsea imefikisha pointi 80, hata kabla ya kucheza inaweza kuiombea Arsenal ipate sare moja tu, kwisha kazi!

Lakini kama kweli Arsenal watakomaa na kushinda mechi zote tano zilizobaki, usisahau Chelsea itakuwa imebakiza mechi nne mkononi, maana yake ni ushindi wa mechi moja au sare tatu, itashindikana kweli?

Soka ina maajabu yake, lakini kuna sehemu inawezekana kunakuwa hakuna nafasi ya maajabu tena badala yake hali halisi ndiyo inakuwa inatawala kila kitu. Kwamba kujihakikishia ubingwa kwa Chelsea ni mechi yao, ikishinda leo.

Mechi dhidi ya Leicester City si rahisi. Kwa takwimu unaweza kudharau kwa kuwa inashika nafasi ya 17 katika msimamo, lakini usisahau inapambana kuokoa ‘uhai’ wake kuepuka kuteremka daraja.

Timu zinazokuwa zinapambana kuwania kubaki katika ligi ni hatari katika mechi za mwisho, Chelsea watakuwa wanalijua hilo na usishangae kuwaona vijana wa Jose Mourinho wakijilinda utafikiri wanacheza na Barcelona. Lakini watashambulia kwa kushitukiza, wakifunga bao moja tu, wapinzani wamekwisha.

Chelsea haina shida ya kuonyesha soka la kuvutia katika mechi zake zilizobaki hadi itakapochukua ubingwa. Hivyo mechi ya leo, kila timu itapambana hadi jasho la mwisho ingawa Leicester ina kumbukumbu ya kuchapwa mabao 2-0 ikiwa ugenini Stamford Bridge. Je, leo italipa? Itaweza kuondoka na pointi tatu dhidi ya Chelsea ‘jeuri’ inayotaka ubingwa.

Mechi
Leicester si ya kudharau kwa kuwa imeshinda mechi zake nne zilizopita, lakini takwimu zinailinda Chelsea kwa kutopoteza mechi zake 13 zilizopita. Chelsea ina 88% ya kufunga mabao ugenini, ina 79% ya kuwa ya kwanza kufunga bao katika mechi zake 33, pia haijafungwa mechi sita za ugenini. Kazi ipo.

LEICESTER                                                 CHELSEA
Mechi 4 za mwisho nyumbani                  Mechi 4 za mwisho ugenini          
Swansea City       2-0                                    0-0    Arsenal
West Ham Utd      2-1                                    0-1         QPR
Hull City                0-0                                    2-3         Hull City
Crystal Palace       0-1                                    0-1         West Ham Utd

MECHI 8 ZA MWISHO:

LEICESTER
Burnley        0-1        Leicester
Leicester        2-0        Swansea City 
West Brom 2-3         Leicester
Leicester        2-1        West Ham
Tottenham 4-3       Leicester
Leicester        0-0        Hull City
Man City        2-0        Leicester
Everton        2-2        Leicester

CHELSEA:
Arsenal         0-0        Chelsea
Chelsea        1-0       Man United
Chelsea        1-0        QPR
Chelsea        2-1        Stoke City
Hull City         2-3        Chelsea
Chelsea        1-1        Southampton
West Ham 0-1        Chelsea
Chelsea        1-1         Burnley

 ZILIPOKUTANA MARA YA MWISHO
Agosti 23:
Chelsea        2-0        Leicester

NAFASI KATIKA MSIMAMO:
Chelsea        1

Leicester        17

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic