Kuelekea mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Yanga dhidi ya Etoile Du Sahel ya
Tunisia utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumamosi.
Chama cha Soka Dar es Salaam (DRFA), kimeitabiria makubwa klabu hiyo ya Jangwani kuvuka
katika kizingiti hicho kigumu kwa mchezo wa nyumbani na ugenini dhidi ya wababe
hao wa Tunisia.
Mwenyekiti wa chama hicho Almasi
Kasongo, amesema ili yanga ifanye vizuri katika mechi hiyo na kuwapa raha
mashabiki wake na watanzania kwa ujumla,ni lazima icheze kwa uangalifu mkubwa
na kukwepa kuendana na style ya kupoozesha mpira wanayoitumia wapinzani katika
mechi za ugenini.
kasongo amelishauri benchi la
ufundi la Yanga chini ya makocha Hans Pluijm na msaidizi wake Charles
Mkwasa, kutumia mbinu ya kushambulia kwa muda wote ili kuwaduwaza wapinzani
ambao wakati mwingine hutumia mbinu ya kufanya mashambulizi ya kushtukiza.
Ametoa wito pia kwa mashabiki wa
soka mkoa wa Dar es salaam na maeneo ya jirani, kujitokeza kwa wingi siku ya
jumamosi kuishangilia Yanga ambao wanaliwakilisha taifa katika mashindano hayo
ya vilabu barani Afrika.
Hata hivyo DRFA inaamini kuwa
Yanga ambayo ni moja ya timu zake zilizopo katika mkoa wa Dar es salaam haina
sababu ya kutofanya vizuri katika mchezo huo, kutokana na kuwa na kikosi kizuri
kilichovisambaratisha katika michuano hiyo vilabu vya BDF ya Botswana pamoja na
Platinum ya Zimbabwe.
IMETOLEWA NA OMAR KATANGA WA DRFA
0 COMMENTS:
Post a Comment