April 16, 2015


Kiungo Mbrazil, Andrey Coutingo ameonyesha uwezo wa juu katika upigaji wa mikwaju ya mipira 'iliyokufa'.


Coutinho hajawa fiti sawasawa baada ya kurejea uwanjani baada ya kukaa nje akisumbuliwa na maumivu, alifanya vema wakati wa upigaji gaulo katika mazoezi ya Yanga.

Yanga inayojiandaa kuivaa Etoile du Sahel ya Tunisia katika michuano ya Kombe la Shirikisho jijini Dar, Jumamosi, imekuwa ikijifua kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar.

Kocha Hans van der Pluijm amekuwa akiwanoa wachezaji wake katika mitindo tofauti kama kucheza kwa kasi, pasi za haraka na upigaji faulo.

Coutinho amekuwa akionyesha uwezo mkubwa sana kwa kupiga mipira mingi aliyofunga au kutoka karibu kabisa na lango.

Kutokana na upigaji wake mzuri, Coutinho amekuwa kivutio kwa mashabiki wengi wanaojitokeza kuangalia mazoezi ya Yanga.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic