April 16, 2015

 
Yanga imeendelea kujifua vikali kujiandaa na mechi yake dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho itapigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga imekuwa ikiendelea kujifua kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar, lakini leo imehamia Uwanja wa Taifa ambao utachezewa mechi hiyo.

Katika mazoezi ya leo Taifa, Yanga ilicheza soka la haraka kujiandaa na Waarabu hao wa Tunisia.
Mara kadhaa, Kocha Hans van der Pluijm na msaidizi wake, Charles Boniface Mkwasa walikuwa wakisisitiza kuhusiana na kucheza soka la kasi.








0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic