Timu ya soka ya Kampuni ya Global Publishers, Global FC, imepata
mwaliko wa kushiriki katika Bonanza la Siku ya Wafanyakazi, Mei Mosi 2015,
linalotarajiwa kufanyika huko Bagamoyo, Pwani.
Hii ni mara ya pili kwa Global kualikwa kwenye bonanza hilo ambalo hufanyika
kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Kilomo, Bagamoyo.
Mratibu wa bonanza hilo, Joseph Ngunangwa ambaye ni mwalimu
kitaaluma, amesema mikakati
yote ya siku hiyo maalum kwa wafanyakazi wote duniani.
“Bonanza
litafunguliwa rasmi saa nane mchana, lakini ukiachana na mechi hiyo pia
kutakuwa na fursa ya kujumuika katika michezo mingine inayoweza kujenga afya na
kufurahia kwa pamoja,” alisema Ngunangwa.







0 COMMENTS:
Post a Comment