Hendrik Johannes Cruijff ‘Johan Cruyff’ ambaye ni kocha mkuu wa
kikosi cha magwiji cha Barcelona anatarajiwa kutua leo saa moja asubuhi.
Magwiji hao wa Barcelona, watatua hapa nchini kwa ajili ya kuvaana
na magwiji wa Tanzania katika mchezo utakaopigwa Aprili 11, mwaka huu kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa waratibu wa ziara hiyo, Said Tully, amesema kocha huyo
anatarajiwa kutua nchini tayari kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa
dhidi ya magwiji wa soka waliowahi kuwika hapo zamani hapa nchini Tanzania.
Tully alisema wakati kocha huyo akitua, wachezaji wanaounda kikosi
cha magwiji wa Barcelona, wanatarajiwa kutua Aprili 7, mwaka huu tayari kwa
mechi hiyo.
Alikitaja kikosi cha magwiji wa Barcelona kinatarajiwa kuundwa na
Patrick Kluivert, Deco, Luis Garcia, Gaizke Mendieta na Edgar Davids kabla ya
siku ya pili yake kwenda Zanzibar baada ya kupata mwaliko wa Rais wa Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Mohammed Shein.
Kwa upande wa kikosi cha magwiji wa Tanzania, kitaundwa na Mohammed
Mwameja, John Mwansasu, Kali Ongala, Salvatory Edward, Yusuf Macho, Bita John,
Victor Costa, Peter Manyika, Nassoro Bwanga na wengine wengi.









0 COMMENTS:
Post a Comment