![]() |
| MASHABIKI WA MABINGWA TANZANIA BARA, AZAM FC AMBAO WANATETEA UBINGWA WAO HUKU WAKIPAMBANA NA VINARA WA LIGI HIYO, YANGA. SIMBA NDIYO WANAOSHIKA NAFASI YA TATU. |
Bodi ya Ligi
ambao ndiyo wasimamizi wa Ligi Kuu Bara, imeweka wazi kuwa kuanzia sasa,
Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (Takukuru) itazichunguza kwa
kina timu tatu zinawania ubingwa wa ligi ambazo ni Simba, Yanga na Azam ili
kukwepa upangaji wa matokeo.
Timu hizo
ndizo zinazopigana kuwania ubingwa wa ligi kuu ambapo zinashika nafasi tatu za
juu na ndiyo maana umuhimu mkubwa umeelekezwa kwao.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Fatuma Abdallah alisema wamegundua kuwa
ligi inapofikia mwishoni kumekuwa na matukio tata, hasa yanayoonekana kuhusishwa
na upangaji wa matokeo.
Alisema kuwa
tangu mwanzoni mwa msimu, Takukuru walikuwa wakiifanya kazi hiyo lakini katika
kipindi hiki wameongeza nguvu kwa kuwa ndicho cha hatari zaidi kufanyika
matukio hayo.
“Tumekuwa
tukifanya kazi na Takukuru ya kuchunguza timu ambazo zinafanya hujuma katika
ligi pamoja na kutoa rushwa kwa muda mrefu lakini sasa tumeongeza nguvu, hasa
katika zile timu tatu za juu kwani hizo zinaweza kufanya vitendo vibaya ili
waweze kutwaa ubingwa,” alisema Fatuma.








0 COMMENTS:
Post a Comment