April 14, 2015

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ameeleza mateso makubwa aliyoyapata kutokana na kuwa majeruhi na kukosa mechi nyingi za msimu uliopita.


Messi amesema ulikuwa msimu mgumu sana kwake kwa kuwa alitamani kucheza na ilishindikana.

Alisema hata aliporudi na kuanza kucheza, bado hakujisikia vizuri na alijaribu kupambana ili asahau hali ile iliyomtesa.

"Nilijaribu kusahau kwa nguvu yaliyonikuta katika msimu uliopita ili niweze kucheza vizuri. Ilikuwa ni ngumu sana kwangu mwanzoni.

“Baadaye niliamua kuinjoy uchezaji wangu, ilinisaidia kusahau na kurejea katika kiwango kizuri.


“Ingawa haikuwa lahisi, naweza kusema ninashukuru kwa kuwa sasa najisikia vizuri,” alisema Messi.

1 COMMENTS:

  1. Hebu mafundi wa Kishwahili wanielimishe. hivi ni 'lahisi' au 'rahisi'. Mwandishi anatumia sana 'lahisi'

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic