April 15, 2015

Tobo mbili alizopigwa beki David Luiz na mshambuliaji Luis Suarez zimezaa mabao mawili na PSG imechezea kipigo cha mabao 3-1 ikiwa nyumbani Paris, Ufaransa.


Mechi hiyo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya nusu fainali ilikuwa tamu na Suarez amefunga mabao mawili, yote akimtoka Luiz na Neymar akafunga moja.

Kwa upande wa PSg walipata bao lao moja kupitia beki Mathieu aliyejifunga baada ya kujaribu kuokoa. Hata hivyo bao hilo limekuwa na utata kuwa apewe aliyepiga shuti au aliyeugonga mpira ukaenda wavuni wakati akiokoa.

PSg inalazimika kushinda bao 2-0 itakapokuwa ugenini Camp Nou ili isonge hadi nusu fainali wakati Barcelona inaonekana kulahisisha kazi.








2 COMMENTS:

  1. sasa hiyo barcelona ugenini imechapwa vipi?
    kagueni vichwa vyenu vya habari!

    ReplyDelete
  2. sasa hiyo barcelona ugenini imechapwa vipi?
    kagueni vichwa vyenu vya habari!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic