Mashabiki wa Liverpool wameandamana
kupinga bei ya tiketi kuwa ni juu sana.
Mashabiki hao walifanya
hivyo kabla ya kusafiri kwenda kuiunga mkono timu yao dhidi ya Hull City katika
mechi ya Ligi Kuu England, leo.
Mashabiki hao walipinga bei
ya tiketi katika Uwanja wa KC kufikia hadi pauni 48.
Walikuwa wakipinga kwamba
bei imekuwa hadi pauni 16, lakini kumekuwa na ongezeko la ghafla ambalo
wanaamini si sahihi.
0 COMMENTS:
Post a Comment