MASHABIKI WA STAND WAKISHEREKEA USHINDI Mechi kati ya Stand United dhidi ya Mtibwa Sugar imemalizika kwa ushindi wa bao 1-0 kwa wenyeji kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. |
Mechi hiyo ililazimika
kuahirishwa hadi leo baada ya mvua kubwa jana huku wenyeji Stand United wakiwa
wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Haruna Chanongo.
Chanongo alifunga bao hilo
mbele ya wachezaji na viongozi wa Simba waliokuwa uwanjani hapo wakisubiri
kucheza dhidi ya Kagera Sugar, leo.
Katika kipande cha mechi
hiyo leo, kila upande ulipoteza nafasi za wazi za kujipatia bao.
Kwa ushindi huo, Stand
imefikisha pointi 24 na kuivuka Mtibwa Sugar inayobaki na 23 baada ya kupoteza
mechi mbili mfululizo, moja ikiwa ni dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja huo wa
Kambarage.
0 COMMENTS:
Post a Comment