Beki wa zamani wa Manchester United na England, Rio Ferdinand
amewasikitisha wapenda soka wengi baada ya kuthibitisha kifo cha mkewe Rebecca.
Rio amesema mwili wa Rebecca umepumzika kwa amani jana kutokana na
ugonjwa wa kansa.
Rebecca ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 34, ameacha watoto
watatu aliozaa na mumewe huyo aliyekuwa beki mahiri.
Rio ambaye sasa anakipiga QPR ameeleza kusikitishwa na kifo hicho
kwa kuwa Rebecca alikuwa mtu muhimu sana katika maisha yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment