May 2, 2015


Yanga wameahidi kupambana hadi tone la mwisho katika mechi ya leo.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari cha Yanga, Jerry Muro amesema kweli kazi si lahisi lakini Yanga haitakata tamaa.

Akizungumza kutoka Sousse, Tunisia, Muro amesema maandalizi ya kila kitu yanakwenda vizuri.
“Watu wanapambana huku, Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga anatuongoza vema kwa kushirikiana na uongozi wa TFF ambao una mwakilishi wao huku.

“Kwa kweli tunapambana, hali si lahisi lakini nakuhakikishia tutapambana hadi mwisho.

“Wachezaji wanalijua hilo na wako tayari, kikubwa tunaomba dua za Watanzania kwa kuwa tunaiwakilisha nchini,” alisema Muro.


Yanga iko Sousse, Tunisia kuivaa Etoile du Sahel katika mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho baada ya sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic