May 2, 2015


Watu wanaoaminika kuwa ni majambazi wamevamia nyumbani kwa msanii Ali Kiba.

Imeelezwa watu wapatao 20 wamevamia nyumbani kwa msanii huyo Kunduchi jijini Dar es Salaam na kuiba mali ikiwa ni pamoja na kuwajeruhi baadhi ya wakati wa nyumba hiyo.

Watu hao waliokuwa na silaha za aina tofauti yakiwemo mapanga, visu na silaha za moto walifanikiwa kuvunja kuingia ndani na kuwadhuru baadhi ya ndugu wa Kiba na kuiba mali na kila kitu ambacho waliweza kubeba, walimpiga na kumtesa mlinzi wa nyumba hiyo wakimtaka awaonyeshe alipo Kiba, hata hivyo hawakufanikiwa kumpata na wakaondoka muda mfupi kabla ya polisi hawajafika nyumbani kwa staa huyo baada ya kupigiwa simu na majirani.


Ikiwa utakuwa na taarifa zozote zitakazosaidia kupatikana kwa majambazi hao, unaweza kutoa taarifa katika kituo cha polisi ulicho karibu nacho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic