Uongozi wa Free State Stars umekubali kumpa Mrisho Ngassa jezi namba 17
ambayo amekuwa akiitumia.
Hiyo inatokana na ombi la kiungo huyo wa zamani wa Yanga ambaye amejiunga
na timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao.
Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Afrika Kusini,
Meneja wa Free State
Stars, Motuba Mokoena amesema Ngassa ameomba kupewa jezi namba 17 ambayo amekuwa akiitumia kutokea Kagera Sugar, Yanga na Simba, pia kikosi cha Taifa Stars.
“Ngassa ameomba tumpe jezi na kumi na saba. Tumeona hilo linawezekana na
tutalifanyia kazi.
“Naweza kusema ni uhakika tutampa jezi hiyo na kazi ya kuwakabidhi jezi
mpya wachezaji wote itafanyika rasmi kesho (leo),” alisema.
Tayari Ngassa yuko Afrika Kusini ambako amejiunga na klabu hiyo kwa
mkataba wa miaka minne.
Baada ya kukabidhiwa jezi, leo, Ngassa ataondoka kwenda kujiunga na
kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinachoshiriki michuano ya Cosafa
inayofanyika nchini humo.
0 COMMENTS:
Post a Comment