Baada
ya kudaiwa kumwagiwa sumu katika vyumba vya kubadilishia nguo katika Uwanja wa
Kambarage, Shinyanga, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amedai kuwa
bado hali yake kiafya si nzuri licha ya kupata matibabu.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita
wakati timu hiyo ilipokuwa ikivaana na Stand United uwanjani hapo na kudaiwa
vyumba vya Ruvu vilipuliziwa vitu vinavyodaiwa kuwa na madhara na kumuathiri
msemaji huyo na kocha wa timu hiyo, Mkenya, Tom Olaba.
“Naendelea
vizuri kiasi lakini mwili wangu bado hauna nguvu na muda mwingine tumbo
linavuruga, nimeshauriwa kunywa sana maji kuhakikisha nakuwa imara kabisa,”
alisema Masau ambaye awali alipatiwa matibabu kwenye Hospitali ya Aghakhan ya
Mwanza lakini kwa sasa yupo Dar akiendelea na matibabu.
Upande
wa Olaba, kocha huyo alipozungumza na gazeti hili alisema: “Nina hasira sana,
naomba nisiongelee masuala ya soka kwa sasa maana naweza kuongea kitu kibaya
kikanisababishia makubwa, lakini naendelea na matibabu, nipo Morogoro, baada ya
siku ile nililazimika kulazwa japokuwa kwa sasa naendelea vizuri.’
0 COMMENTS:
Post a Comment