Simba imeanza mchakato wakusaka wachezaji katika nchi mbalimbali barani Afrika.
Baachi ya nchi ambazo zimeelezwa kuwa Simba inasaka wachezaji ni pamoja na Ghana, Nigeria, Rwanda, Burundi na Kenya.
Simba inafanya hivyo ikiwa ni siku moja tu baada ya kuachana na wachezaji Waganda wake watatu, Simon na Dan Sserunkuma pamoja na Joseph Owino.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema wanaendelea kusaka wachezaji katika nchi hizo.
"Watakuja kufanya majaribio, watakaokuwa na uwezo basi watapata nafasi. Tumeanza kazi hiyo mara moja baada ya kuachana na Sserunkuma na Owino na sasa tuna nafasi ya kusajili.
"Kweli, tunaweza kuacha tena na tena lakini lengo ni kupata watu sahihi," alisema Hans Poppe.
Simba imemaliza Ligi Kuu Bara ikiwa katika nafasi ya tatu, huku ikionekana uongozi umepania kubeba ubingwa msimu ujao.
Hata hivyo, inaonyesha ni lazima kuwe na umakini mkubwa katika usajili wa msimu ujao ili kujiimarisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment