May 6, 2015

Lionel Messi ameonyesha kweli anaweza, kweli ni mchezaji wa “dunia” baada ya kufunga mabao mawili na kutengeneza moja na kuiwezesha Barcelona kushinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Bayern Munich.


Katika mchezo huo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, Messi amefunga mabao hayo mawili kwa uwezo binafsi wakati Barcelona ilionekana imeshindwa kuupennya ukuta wa Bayern iliyokuwa ugenini.

Mabao hayo mawili yalionyesha kuwachanganya mabingwa hao wa Ujerumani wanaofundishwa na Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Gaurdiola na kuwasababisha watoe bao la tatu lililofungwa kwa ulaini na Neymar.

Bayern wanalazimika kujipanga ili kushinda zaidi ya mabao matatu katika mechi itakayopigwa mjini Munich.













0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic