May 2, 2015

 
HANS POPPE
 Simba itafanya kazi ya kufuatilia kiwango cha mshambuliaji Patrick Kiongera ambaye ameanza kuichezea timu ya KCB.


Kazi hiyo itafanywa na watu maalum na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema watafanya hivyo ili kujiridhisha na kiwango chake.
KIONGERA

"Kweli tumekubaliana kumrudisha Kiongera. Yeye bado ni mchezaji wetu lakini alipoumia, tumemtibu na baadaye tumempeleka kwa mkopo Kenya.

"Tutakachofanya ni kuangalia kiwango chake anapokuwa anaichezea timu hiyo kwenye Ligi Kuu Kenya. Tukiridhishwa, basi atarudi.

"Tumekuwa makini na kwenye mkataba hilo suala la kiwango tumeliweka," alisema Hans Poppe.

Simba ilimpeleka mshambuliaji huyo kwenye kutibiwa India ikiwa ni baada ya kuumia katika mechi ya kwanza kabisa ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union.

Sasa amekuwa kati ya wachezaji wa kigeni wanaopewa nafasi kubwa katika listi ya watano msimu ujao. Lakini kamati hiyo chini ya Hans Poppe imeamua kupata uhakika wa kiwango chake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic