CHANONGO AKIWA NA WACHEZAJI WA STAND. |
Uongozi wa Yanga,
sasa umeamua kuimaliza ishu ya kiungo
Haruna Chanongo kwa kusema, imeachana naye kabisa.
Msimu uliopita, Chanongo aliichezea Stand United kwa mkopo akitokea Simba ambayo iliamua kumshusha ikidai hakuwa na kiwango kizuri.
Katibu Mkuu wa
Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema wameachana naye.
“Kweli tumeamua
kuachana kabisa na Chanongo, sasa tunaendelea na taratibu nyingine,” alisema.
Dk Tiboroha
alisema walikuwa kweli katika mazungumzo na Chanongo, lakini inaonekana kuna
mambo kadhaa yameshindikana.
Amesema kutokana
na mambo hayo kushindikana, basi wao wataendelea na mambo mengine na Chanongo
wanamuacha aendelee na yake.
Habari za ndani
kutoka ndani ya Yanga, zimeeleza kuwa walikuwa wamefikia makubaliano na
Chanongo lakini baadaye akabadilika na kutaka fedha zaidi.
“Alitaka fedha,
akakubaliwa. Kabla ya kusaini, ghafla akabadili tena na kutaka zaidi,”
kilieleza chanzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment