May 26, 2015




Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amemvulia uvivu meneja wa kiungo wao, Ramadhani Singano ‘Messi’ kwamba analazimika kuwa makini.


Hans Poppe amesema meneja huyo anapaswa kuwa makini kutokana na maneno aliyoyatoa kwamba mkataba wa mchezaji wake ‘umechezewa’.

“Kwa kweli anapaswa kuwa makini sana, maneno anayoyazungumza hayana ukweli na anapaswa awe na uhakika.

“Anaposema kuna ujanja umefanyika katika mkataba huo wakati uko TFF, maana yake TFF wanahusika kuufanyia ujanja.

“Tumegushi saini, tumegushi na dole gumba. Sidhani kama ni jambo zuri kuzungumza tu hayo mambo.

“Anapaswa kuwa makini, nasema hivi kumuasa lakini bado naweza kusema simtambui kwa kuwa sijui yeye Messi ana meneja na wala hajawahi kuutambulisha uongozi wa Simba,” alisema Hans Poppe.

Meneja huyo amekuwa akilalama kwamba mkataba wa Simba na Messi unapaswa kulazimika msimu huu lakini ulio TFF unaonyesha unamalizika mwakani yaani 2016.

Lakini ajabu Messi, ameshindwa kuonyesha nakala ya mkataba wake ambayo ingeweza kuonyesha kama kweli Simba wamekosea au la.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic