Kila
kukicha Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe anatamba
kwamba atamsajili winga Simon Msuva wa Yanga, kumbe jeuri yake inatokana na
wazazi wa mchezaji huyo.
Msuva
aliliambia Championi Jumamosi kuwa, wazazi wake wote ni wapenzi wa Simba na
kuna wakati akiwa Moro United kabla ya kutua Yanga baba yake Happygod Msuva
alitaka kumpeleka Simba lakini ikashindikana.
“Baba
alitaka kunipeleka Simba wakati ule, lakini kiongozi mmoja alikataa akiniambia
nilikuwa mdogo ndipo nilipotua Yanga sasa bado mazungumzo yao na baba
yanaendelea na wanajipa matumaini ya kunisajili kitu ambacho si sahihi,”
alisema Msuva.
Mara
kadhaa Hans Poppe amekaririwa na vyombo vya habari akisema lazima Msuva
asajiliwe na Simba na kauli yake ameirudia hivi karibuni baada ya winga huyo
kufikisha mabao 17 na kuongoza kwa ufungaji katika ligi kuu.
Kwa
sasa Msuva yupo Tunisia na kikosi cha Yanga ambacho leo Jumamosi usiku
kitacheza mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho na Etoile du Sahel jijini
Sousse.
0 COMMENTS:
Post a Comment