May 2, 2015


Hii sasa kasheshe kwani nahodha na beki wa kati wa Simba, Hassan Isihaka, mkataba wake unaelekea kwisha na amesema anataka apewe mwingine mnono kama wa Jonas Mkude.


Wakati Isihaka akitingisha kiberiti, kipa mkongwe Ivo Mapunda naye amesusa kwa kusema hataukumbusha tena uongozi kuhusu mkataba wake mpya kwani amechoka kupigwa danadana.

Isihaka ambaye nyota yake imewaka msimu huu akicheza sambamba na Juuko Murshid katika beki ya kati, amesema Simba inabidi itoe kiasi kikubwa cha fedha ili asaini mkataba mpya kwani na yeye ni mtu muhimu kikosini.

 “Mimi, Mkude na nyota wengine tumesota wote Simba na kuifikisha timu ilipo sasa, tulicheza kwa moyo wakati mwingine katika mazingira magumu hivyo sasa ni wakati wa kuona matunda yake,” alisema Isihaka.

Kauli ya Isihaka inamaanisha anataka apewe mkataba mnono kama ule aliopewa Mkude mwaka jana wenye thamani ya Sh milioni 60 ambapo alilipwa fedha nusu yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic