Pamoja
na kiungo wa Klabu ya Simba, Shabani Kisiga kuonyesha nia ya kurejea kundini
kuitumikia klabu hiyo, uongozi wa timu hiyo umefungua kinywa na kudai kuwa
hauwezi kumrudisha mchezaji huyo hata kwa dawa.
Uongozi
huo umesema hayo baada ya kudai kuwa wamelisikia tamko la mchezaji huyo, lakini
wao wanaona kama anawakejeli kwa sababu walimpa fursa mara mbili ya kujieleza
na kushindwa kufika, kitendo kilichoashiria ni kama dharau.
Taarifa zinaeleza, Kisiga amekuwa akifanya juhudi za kuwashawishi viongozi ili arejee. Lakini amekataliwa katakata na sasa Simba inaangalia mipango ya kupata wachezaji watakaowaondoa walipo sasa.
"Lengo lilikuwa ni kutaka kutengeneza Simba iliyo imara, tuliamini Kisiga ni wachezaji wakongwe na watasaidia kuwaongoza vijana. Lakini haikuwa hivyo.
“Msimu
ujao tunataka kuwa makini sana katika suala zima la usajili litakalozingatia
zaidi nidhamu, kwani hata kama mchezaji ukiwa bora bila nidhamu ni sawa na
bure,” kilieleza chanzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment