MAKAPU (KUSHOTO) AKIPAMBANA NA AJIBU... |
Huku
kikosi cha Taifa Stars leo Jumatano kikitatarajiwa kushuka dimbani kumenyana na
Madagascar katika mchezo wa pili wa michuano ya Cosafa inayofanyika nchini
Afrika Kusini, timu hiyo inatarajia kukosa huduma ya kiungo mkabaji wa Yanga,
Said Juma Makapu ambaye amerudishwa nchini kutokana na kuwa majeruhi.
Makapu,
mashabiki mbalimbali wa soka hapa nchini wanamfananisha na kiungo wa timu ya
Chelsea ya England, Nemanja Matic.
Akizungumzia
juu ya jambo hilo, Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Selestine
Mwesigwa, alisema mchezaji huyo amerudishwa nchini baada ya kuonekana ana
majeraha yanayomsumbua na hayawezi kupona haraka na kupata fursa ya kuitumikia
timu hiyo.
“Makapu
anarudishwa Dar, ana majeraha ambayo aliyapata kwenye ligi na hivyo inaonekana
hawezi kuitumikia timu hiyo huku Afrika Kusini,” alisema Mwesigwa.
Katika
hatua nyingine, Mwesigwa alisema msimu ujao wa ligi kutakuwa na sheria pamoja
na kanuni nyingi mpya baada ya kutoa fursa kwa timu zinazoshiriki kupendekeza
maoni yao juu ya kipi kiongezwe na kipi kitolewe ili kunogesha ligi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment