Kumbe hata Wazungu wanajua ile ishu ya “asui
mwombee njaa!”. Maana Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesisitiza kwamba
anatamani Azam iboronge michezo yote iliyobaki.
Kopunovic raia wa Serbia anaamini kama Simba
itashinda mechi zote zilizobaki, Azam ikafulia, basi wao watabeba nafasi ya
pili.
“Ndiyo, dua mbaya kwa mpinzani wako si
vibaya. Si dua mbaya aumie, nazungumzie apoteze mechi,” alisema huku
akitabasamu.
Simba iko katika nafasi ya tatu ikiwa na
pointi 44, wakati Azam FC iko katika nafasi ya pili ikiwa na nafasi 45.
Kesho Azam FC inashuka dimbani
kucheza na Yanga
0 COMMENTS:
Post a Comment