Kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand United, ndiyo kimeishusha
Ruvu Shooting hadi daraja la kwanza.
Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amekubali kipigo lakini
akasisitiza: “Ilikuwa utafikiri hawako Tanzania.”
“Walikuja vijana na mapanga hadi hotelini kwetu, walitutishia. Ikafikia
tukashitaki kwa mabosi wa polisi lakini hakuna aliyetusaidia.
“Nikalazimika kuwasiliana na kuwasiliana na makao makuu ya
Polisi kupitia Chagonja, ndiyo tukapata msaada.
“Lakini tulipoingia vyumbani, mambo yalikuwa mazuri. Tulipotoka kwenda
kupasha mwili, kosa kubwa.
“Tumerudi vyumbani kuna harufu kali ya dawa iliyopuliziwa kwa ajili ya kupunguza nguvu ya mwili. Hii
imechangia kwa kiasi kikubwa kuwaumiza vijana. Kamisaa ameona, nimemuita na
harufu kaivuta pia, waandishi wameona.
“Achana na hivyo, tulipambana sana uwanjani lakini mwamuzi
alikuwa kama ni mtu aliyepewa maagizo kwamba sisi lazima tufungwe,” alisema
Masau ambaye timu yake itacheza daraja la kwanza msimu ujao.








0 COMMENTS:
Post a Comment