Kocha
wa zamani wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, ameweka wazi kuwa yupo tayari
kuinoa Mwadui FC kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara endapo tu
watakubaliana masuala ya mkataba.
Phiri
ambaye aliipa Simba ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2009/10 bila kupoteza
mchezo wowote, kwa sasa hana timu tangu atimuliwe na Simba mwishoni mwa mwaka
jana na sasa yupo nchini kwao akijishughulisha na shughuli nyingine nje ya
soka.
Phiri,
amesema kuwa: “Kwa sasa sina timu, nipo ninaendelea na
shughuli zangu binafsi, Mwadui sijaijua vizuri, ninaisikia juujuu tu, lakini
mimi nipo tayari kufanya nao kazi endapo tutakubaliana masuala ya mkataba na
maslahi kwani napenda kufanya kazi Tanzania.”
Mpaka
sasa viongozi wa Mwadui FC wapo njia panda kama waendelee na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’
ambaye alipata kazi kwa muda Coastal Union ya Tanga au waajiri kocha mwingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment