Wakati majaaliwa ya Kocha Goran Kopunovic raia wa Serbia yakiwa hayajulikani
kuifundisha Simba, klabu hiyo imeweka wazi kuwa inatarajiwa kufanya usaili wa
makocha wengine kutoka nchini Ufaransa, Bulgaria, Senegal na Serbia.
Simba
imetoa tamko hilo kutokana na mkanganyiko wa masuala ya maslahi ya mkataba mpya
kati ya Kopunovic na klabu hiyo ambapo imeelezwa kuwa Simba haipo tayari
kuendelea kuwa naye ikiwa atashikilia msimamo wa kuhitaji maslahi wanayoona ni
makubwa tofauti na bajeti yao.
Akizungumzia
suala hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe,
alisema mipango ya kuleta kocha mpya ipo ikiwa watashindwana rasmi na Mserbia
huyo na kuzitaja nchi hizo kuwa ndiyo zinazoweza kutoa kocha wao.
“Ikiwa
tutashindwana na Kopunovic, kuna makocha kutoka nchi nyingi tu, wapo kutoka
Ufaransa, Senegal, Bulgaria na hata Serbia huko ambapo anatokea yeye,” alisema
Hans Poppe.
Kuhusu
usajili mpya ikiwa ni siku moja baada ya kutangaza wazi kutoendelea kuwa na
beki Joseph Owino na Dan Sserunkuma kiongozi huyo alisema nako pia kuna
wachezaji kutoka nchi kadhaa ambao wanajiandaa kuwaleta.
“Kuna
wachezaji kutoka Ghana, Burundi, Kenya, Rwanda na Nigeria, kote huko
tumeshapata maombi na mipango inafanyika kuja kufanya majaribio,” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment