HANS POPPE |
Bosi wa kamati ya usajili
ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema Kocha Goran Kopunovic ana kila sababu ya
kuchagua, abaki au aende.
Hans Poppe amesema
mazungumzo yao na Kopunovic ametaka dau kubwa hadi Sh milioni 28 kwa mwezi kama
mshahara.
“Kweli bado hatujaelewana
katika suala la maslahi. Sisi tunataka aendelee kubaki, lakini kwa fedha
anayotaka hatuwezi kutoa.
“Kwa mwezi wadhamini
wanatupa shilingi milioni 30 kwa mwezi kulipa wachezaji mishahara, yeye anataka
achukue yote milioni 28.
“Hivyo tumemuachia yeye
aamue kwa fedha ambazo tumemuambia. Kama hataweza basi atakwenda,” alisema Hans
Poppe.
Taarifa za ndani ya Simba
zimeeleza, kocha huyo ametaka mshahara wake upande kutoka dola 5,000 hadi dola
14,000 kwa mwezi.
Hali ambayo imeifanya Simba
ishindwe kutoa fedha hizo na kusisitiza ikishindikana basi wataendelea kutafuta
makocha wengine.
0 COMMENTS:
Post a Comment