NYUMBA YAKE AMBAYO AMEIINGIZA SOKONIMshambukiaji nyota na kinda wa Liverpool, Raheem Sterling ameanza maandalizi ya kuipiga bei nyumba yake. |
Sterling yuko katika maandalizi ya kuipiga bei
nyumba yake jijini Liverpool na inaelezwa ameanza kutafuta nyumba jijini
London.
Uamuzi wa kutaka kuiuza nyumba hiyo na kuanza
kutafuta nyingine jijini London ni dalili kwamba kweli anakaribia kuondoka na
kujiunga na kati ya timu mbili; Chelsea au Arsenal.
Kinda huyo kwenye miaka 20 amehusishwa na
kujiunga na timu hizo mbili za London mara tu baada ya kukataa ofa ya Liverpool
ya pauni 90,000 kwa wiki.
0 COMMENTS:
Post a Comment