May 25, 2015

NDEMLA AKISAINI MKATABA WA MIAKA MITATU KUICHEZEA SIMBA MBELE YA RAIS WA KLABU HIYO, EVANS AVEVA, LEO.
 Simba imekata mzizi wa fitna baada ya kumpa mkataba wa miaka mitatu mingine kiungo wake Said Ndemla shughuli iliyofanyika jijini Dar es Salaam, leo.

Ndemla amesaini mkataba wa miaka mitatu mingine kuendelea kuichezea Simba ambayo amekuwa akiitumikia kama mchezaji kinda.
Awali kulikuwa na taarifa za Ndemla kuwaniwa na Yanga baada ya kusikia amebakiza mwaka mmoja tu na Simba.

Lakini Msimbazi, wameifuta ndoto hiyo baada ya kuhakikisha Ndemla anaendelea kubaki Msimbazi zaidi na zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic