Kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola alionekana
akizungumza mambo kadhaa na Lionel Messi wakati wa mapumziko.
Mechi kati ya Bayern Munich dhidi ya Barcelona
ilikuwa mapumziko na wakati wanakwenda vyumbani wawili hao wakaanza kupiga
stori.
Utafikiri Guardiola alikuwa akimuambia Messi: “Usiniue
mwanangu.”
Maana Messi alifunga mabao mawili mjini Barcelona na
kuisaidia timu yake kushinda kwa 3-0 ambazo zimesongesha mbele hadi kwenye
fainali.
Kwani Bayern Munich imeshinda 3-2 lakini
hazijaiwezesha kusonga mbele.
Kabla ya kutua Munich, Guardiola alikuwa Barcelona
na mchezaji wake tegemeo alikuwa ni Messi.
0 COMMENTS:
Post a Comment