Mshambuliaji wa zamani wa
Yanga, Said Bahanuzi amesema anataka Yanga imlipe kitita cha Sh milioni 17.
Bahanuzi amesema anahitaji
kulipwa fedha hizo baada ya Yanga kukatisha mkataba wake.
“Tayari suala hilo
linashughulikiwa na mwanasheria. Wanajua kuwa wanatakiwa kunilipa, hivyo
naendelea kusubiri kutoka kwao,” alisema.
Hata hivyo Yanga
ilishafafanua suala hilo na kusema Bahanuzi alicheza chini ya kiwango kitu
ambacho kimkataba wanakuwa na uamuzi wa kuendelea naye au la.
Bahanuzi aliwahi kuisaidia
Yanga kubeba Kombe la Kagame mwaka 2012 Yanga ikiwa chini ya Kocha Tom
Saintfiet ambaye sasa ni kocha wa Togo.
0 COMMENTS:
Post a Comment