Yanga imesema haina sababu
zozote za kumzuia kipa Juma Kaseja kujiunga na timu nyingine kwa kuwa kweli
haimhitaji.
Awali kulikuwa na taarifa kwamba Yanga inamfanyia Kaseja ntomanyongo kwa kushindwa kumuachia aende timu nyingine.
Lakini Mwanasheria wa
Yanga, Frank Chacha amesema Kaseja yuko huru kujiunga na timu nyingine wakati
kesi yao dhidi yake ikiendelea.
“Kaseja ameamua kuacha kazi
mwenyewe, sasa si mwajiriwa wa Yanga na sisi tumefungua kesi. Si kweli hatutaki
ajiunge na timu nyingine na wala hatuna sababu ya kumzuia.
“Kama atapata timu na kuna
taratibu za kufanya, azifuate na kujiunga nayo. Sisi kesi yetu itaendelea
mahakamani hadi hapo hukumu itakapotoka.
“Huenda kama tutashinda,
basi akatulipa kupitia fedha anazolipwa. Hivyo ni vizuri kuliko kuendelea kukaa
kijiweni kwa kuwa sisi tunamzuia,” alisema Chacha.
Kauli ya mwanasheria huyo
imefuta utata kwamba Yanga ilikuwa ikimfanyia Kaseja ntimanyongo kwa kumzuia
asisajiliwe na timu nyingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment