Kocha Mkuu wa
Misri, Hector Cuper ametamba kuwa kikosi chake kilikuwa na nafasi ya kuinga
Tanzania angalau mabao saba.
Cuper raia wa
Argentina amesema walipoteza nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza.
“Hilo ndiyo
lilikuwa tatizo kubwa sana, niliona wachezaji walikuwa na poresha ya juu. Ndiyo
maana tulipokwenda mapumziko nikawaambia watulie.
“Hawakuwa na
haja ya presha kubwa, niliwashauri kucheza soka kama wanavyocheza lakini
wafunge na hilo wakalitekeleza,” alisema.
Misri
iliifunga Taifa Stars kwa mabao 3-0 katika mabao yaliyopatikana katika kipindi
cha pili tu.
Misri ipo
kundi moja na Tanzania, Nigeria na Chad na kocha huyo aliyewahi kuinoa Valencia
ya Hispania, amejigamba kuwa Misri ina kikosi kipana zaidi ya timu nyingine
katika kundi hilo.









0 COMMENTS:
Post a Comment